Mandzukic:Klabu ya Juventus imeshinda mbio za kumsajili mshambuliaji Atletico Madrid Mario Mandzukic 29 baada ya vilabu vyote viwili kukubaliana ada ya €18m ambayo italipwa kwa mikupuo miwili.Mandzukic anatua Juventus ili kuziba
nafasi ya Carlos Teves aliye mbioni kutua Boca Juniors ya kwao Argentina.
Ospina:Klabu ya Arsenal imekubali ofa ya £4m toka klabu ya Fernebhace ya Uturuki kwa ajili ya mlinza mlango wake David Ospina,26.Arsenal ina muuza Ospina ili kutoa nafasi kwa mlinda mlango Peter Cech anayetarijiwa kutua klabuni hapo siku chache zijazo.
Remy:Klabu ya Chelsea imeviambia vilabu vyote vinavyomtaka mshambuliaji wake Mfaransa Loic Remy 28 vijiandae kutoa kitita cha £15m vinginevyo nyota huyo ataendelea kukipiga Stamford Blidge.
Bonucci:Klabu ya Real Madrid inajipanga kumuuza mlinzi wake Raphael Varane kwenda England kwa ada ya €40m kisha kutumia €30m kumsajili mlinzi wa Juventus Leonardo Bonucci.
Simeone:Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone amesema wachezaji Diego Godin na Koke ndiye pekee hawauzwi lakini wengine wote wako sokoni.
Miyaichi:Klabu ya Arsenal imeripotiwa kuachana na wachezaji wake wawili Ryo Miyaichi aliyetua St.Pauli na Ajayi alihamia Cardiff City inayoshiriki Championship.
Mikel:Kiungo John Obi Mikel yuko njiani kutua katika klabu ya Fernabhce ya Uturuki baada ya klabu hiyo kuripotiwa kuanza mazungumzo na klabu ya Chelsea inayommiliki nyota huyo toka Nigeria.
Soares:Klabu ya Southampton imekamilisha usajili wa mlinzi wa kulia wa klabu ya Sporting Lisbon Cedric Soares.Soares amesaini mkataba wa miaka minne ya kuwachezea wakali hao wa St.Mary's lakini ada yake ya uhamisho haijawekwa wazi.
0 comments:
Post a Comment