728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 22, 2015

    MKUDE APEWA WIKI MBILI SAUZ

     
    HATIMAYE sasa yametimia na rasmi kiungo mkabaji wa Simba SC, Jonas Mkude, anatarajia kuondoka nchini Alhamisi ya wiki hii kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya wikimbili kwenye kikosi cha Bidvest Wits
    ya Afrika Kusini ‘Sauz’.

    Mipango hiyo ya mchezaji huyo ilianza kuiva tangu akiwa kambini nchini Ethiopia na kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars ambapo sasa inaonekana yametimia.

    Imeelezwa kuwa wakala kutoka nchini Uingereza anayejulikana kwa jina la Mitchelle Paul ndiye anayesuka mipango yote na tayari ameshazungumza na uongozi wa Simba kuhusiana na masuala hayo na wamekubaliana kuwa kama kijana atafuzu basi watakaa chini ya Wits kumalizana.

    Aidha, Wits waliomaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya Sauz nyuma ya mabingwa Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundowns, walitaka kumpa Mkude muda wa mwezi mzima kufanya majaribio lakini imeelezwa kuwa Paul alilikataa suala hilo na kupendekeza wiki mbili pekee.

    Baada ya majaribio hayo, Mkude anatarajia kurejea nchini kuanzia Julai 2 au 3, mwaka huu kwa ajili ya kusikilizia majibu yake.
    “Nashukuru mambo yanakwenda vizuri na safari imeiva, natarajia kuondoka Alhamisi hii majira ya alasiri na nitakwenda Sauz kufanya majaribio yangu kwa muda wa wiki mbili kisha nitarejea nchini Julai mwanzoni kuanzia tarehe 2 au 3 kwa ajili ya kusikilizia majibu,” alisema Mkude.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MKUDE APEWA WIKI MBILI SAUZ Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top