Kiungo mkongwe, Shabani Kisiga amesaini mwaka mmoja kuichezea Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
Kisiga aliyewahi kung’ara na Simba na Mtibwa Sugar,amesaini kujiunga na Ruvu Shooting leo.Msemaji wa Shooting, Masau Bwire amesema kwa sasa tayari Kisiga ni mchezaji wao.
“Tunaendelea kujiimarisha,kweli Kisiga tumemsajili kwa mkataba wa mwaka mmoja,” alisema Masau.
Kiungo huyo aliondoka Simba baada ya kushindwa kuelewana na uongozi na ilielezwa chanzo alikuwa yeye baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu mara kadhaa kwa maafisa wa benchi la ufundi.
0 comments:
Post a Comment