728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 28, 2015

    COPA AMERICA:BRAZIL YATUPWA NJE,NUSU FAINALI KUANZA KESHO JUMATATU

    Timu ya taifa ya Brazil imetupwa nje ya michuano ya Copa America baada ya kukubali kichapo cha penati 4-3 toka kwa timu ya taifa ya Paraguay.
    Mpaka dakika 90 za mchezo huo wa robo fainali zinakwisha timu hizo zilikuwa sare ya goli 1-1,Brazil walipata goli lao dakika ya 15 kupit
    ia kwa winga Robinho kisha Paraguay kusawazisha dakika ya 72 kupitia mkwaju wa penati uliopigwa na Derlis Gonzalez baada ya mlinzi Thiago Silva kuunawa mpira katika eneo la hatari.
    HISTORIA
    Historia:Kwa mara ya kwanza katika michuano ya Copa America makocha wote walioingiza timu katika hatua ya nusu fainali ni raia wa Argentina.Makocha hao ni Jorge Sampaoli, Ricardo Gareca, Tata Martino na  Ramon Angel Díaz

    VIKOSI VILIVYOKUWA
    Brazil - Jefferson, Alves , Thiago,
    Miranda, Luis, Elias, Fernandinho,
    Willian , Coutinho, Firmino, Robinho.
    Akiba - Ribeiro, Tardelli, Costa.
    Paraguay - Villar, Valdez, Silva, Aguilar, Piris, Caceres, Aranda, Gonzalez,
    Benitez, Santa Cruz , Valdez.Akiba-
    Martinez , Bobadilla,Romero

    NUSU FAINALI
    Jumatatu Juni 29:Chile v Peru (Saa 8:30 Usiku)
    Jumanne Juni 30:Argentina v Paraguay (Saa 8:30 Usiku)

    MSHINDI WA 3:Ijumaa Julai 3
    (Saa 8:30 Usiku)

    FAINALI:Jumamosi Julai 4
    (Saa 5 Usiku)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA:BRAZIL YATUPWA NJE,NUSU FAINALI KUANZA KESHO JUMATATU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top