Habari na Paul Manjale
Kiungo wa klabu ya Juventus na timu ya taifa ya Chile Arturo Vidal 28 amenusurika kifo jana jumanne usiku baada ya gari yake kugongana na gari jingine
katika jiji la Santiago.
Vidal akiwa na mkewe Maria Teresa Matus wakitoka kula starehe katika Casino moja maarufu walikutwa na ajari hiyo baada ya Vidal kushindwa kulidhibiti gari alilokuwa akiliendesha kutokana na kuzidiwa na pombe.
Afisa mmoja wa polisi aliyejulikana kwa jina la Ricardo Gonzalez alisema "Dereva wa gari jekundu alikuwa amelewa sana"
Vidal alikimbizwa katika hospital ya San Luis de Buin kupata matibabu baada ya kupata majeraha madogo madogo.
Baadae nyota huyo wa Juventus alionekana akiwa ndani ya gari la porisi akipelekwa kituoni kwa mahojiano zaidi.
0 comments:
Post a Comment