728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 16, 2015

    FALCAO ATUA CHELSEA,SOTON/STOKE ZASAJILI WAHISPANIA



    Falcao:Vilabu vya Chelsea na AS Monaco vimefikia makubaliano juu ya usajili wa mshambuliaji Radamel Falcao kwa mkopo wa msimu
    mmoja.Falcao atajiunga na Chelsea baada ya michuano ya Copa America.

    Cech:Klabu ya Chelsea imekubali kumuuza mlinda mlango wake Peter Cech kwenda katika klabu ya Arsenal kwa kitita cha £11m.Dili hili litakamilika mapema baada ya Chelsea kumnasa mlinda mlango mpya kati ya  Green au Asmir Begovic.

    Tripper:Klabu ya Tottenham iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kulia wa klabu ya Burnley Kieran Trippier kwa kitita cha £3.5m.

    Joselu:Klabu ya Stoke City ndani ya masaa 24 yajayo itatangaza kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari wa klabu ya Hannover 96 Joselu kwa ada ya €8m.

    Juanmi:Southampton imekamilisha usajili wa mshambuliaji Juanmi (Juan Miguel Jimenez Lopez) 22 toka klabu ya Malaga kwa mkataba wa miaka minne.

    Verratti:Barcelona imesema itafikiria kumsajili kiungo wa Paris Saint Germain Marco Verratti ikiwa itashindwa kumsajili kiungo Paul Pogba wa Juventus.(Daily Mirror)

    Jenkinson:Klabu ya Sunderland imeshinda mbio za kumsajili kwa mkopo wa msimu mmoja mlinzi wa kulia wa klabu ya Arsenal Carl Jenkinson.Sunderland imemnasa Jenkinson baada ya kuvishinda vilabu vya West Ham na Southampton.

    Witsel:Kiungo wa Zenit Axel Witsel (26) ameripotiwa kusakwa na vilabu vya Chelsea na Manchester United huku Juventus nao wakihusishwa kumtaka Mbelgiji huyo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: FALCAO ATUA CHELSEA,SOTON/STOKE ZASAJILI WAHISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top