728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 30, 2015

    COPA AMERICA:CHILE YATINGA FAINALI BAADA YA MIAKA 28,KESHO NI ARGENTINA v PARAGUAY

    Santiago,Chile

    Timu ya taifa ya Chile imekuwa ya kwanza kukata tiketi ya kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Copa America baada ya kuibugiza timu ya taifa ya Peru kwa jumla ya goli 2-1katika nusu fainali kali iliyopigwa usiku wa kuamkia leo.

    Katika mchezo
    huo uliopigwa katika dimba la Estadio Naciona jijini Santiago,Chile walipata goli la kuongoza dakika ya 27 kupitia kwa mshambuliaji wake Eduardo Vargas baada ya kuuwahi mpira wa winga Alex Sanchez uliogonga mwamba na kufunga kirahisi.

    Baada ya goli hilo Peru walichachamaa na kupanikiwa kusawazisha goli dakika ya 60 baada ya mlinzi wa Chile Gary Medel kujifunga katika harakati za kuokoa krosi ya Luis Advincula.

    Dakika nne baade Chile walipata goli la pili na la ushindi kupitia kwa mfungaji yule yule Eduardo Vargas baada ya kupiga shuti kali la mbali lililomshinda mlinda mlango wa Peru Sergio Gelesse na kujaa wavuni.

    Kufuatia ushindi huo Chile imefanikiwa kutinga fainali baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho miaka 28 iliyopita huku ikiwa haijawahi kushinda taji hilo tangu lilipoanzishwa miaka 99 iliyopita.

    Kesho jumatano nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itapigwa kati ya Argentina itakayopepetana na Paraguay
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: COPA AMERICA:CHILE YATINGA FAINALI BAADA YA MIAKA 28,KESHO NI ARGENTINA v PARAGUAY Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top