728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 25, 2015

    USAJILI:DE GEA AIPIGA BEI NYUMBA YAKE TAYARI KUTIMKA,MOURINHO AKOMAA NA BABA RAHMAN

    De Gea:Mlinda mlango wa klabu ya Manchester United David De Gea ameripotiwa kutafuta mteja wa kuinunua nyumba yake baada ya kuiweka mtandaoni nyumba hiyo iliyoko maeneo ya Altringham Manchester hii ikiwa ni ishara
    ya kujiandaa kutua katika klabu ya Real Madrid ya nyumbani kwao Hispania.De Gea anaiuza nyumba hiyo kwa kitita cha £2,750,000.
    Clyne:Klabu ya Liverpool iko katika nafasi nzuri ya kumsajili mlinzi Nathaniel Clyne baada ya klabu yake Southampton kukubali ofa ya £12.5m

    Dragomir:Klabu ya Arsenal imemsajili kiungo kinda wa klabu ya Poli Timisoara ya Romania Vlad Dragomir 16 kwa ada ya £71,000.Dragomir ni nahodha wa kikosi cha U-16 ya timu ya taifa ya Romania.
    Baba:Klabu ya Chelsea imetuma ofa ya £10.6m kwa klabu ya FC Augsburg kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa klabu hiyo Baba Rahman,20. (Express)
    Costa:Klabu ya Bayern Munich imeshinda mbio za kumsajili winga Douglas Costa wa klabu ya Shakhtar Donetsk baada ya ofa yake ya £25m kukubaliwa na miamba hiyo ya Ukraine.

    Nani:Klabu ya Fenerbahce inakaribia kumsajili winga wa klabu ya Manchester United Luis Nani from Manchester kwa ada ya £4.3m baada ya kufikia maslahi binafsi na nyota huyo aliyekuwa kwa mkopo katika klabu ya Sporting Lisbon.
    Deulofeu:Klabu ya Everton leo inatarajia kutangaza kumsajili mshambuliaji kinda Gerard Deulofeu (20) toka klabu ya FC Barcelona kwa ada ya £5m.
    Teves:Katibu mkuu wa klabu ya Boca Junior Cesar Martucci  imekiambia kituo kimoja cha Argentina kuwa usajili wa mshambuliaji Carlos Tevez 30 toka Juventus kuja klabuni hapo umekamilika kinachosubiriwa na kufanyiwa vipimo kwa nyota huyo aliyeko Chile katika michuano ya Copa America.
    Nzonzi:Klabu ya Leicester imetuma ofa ya  £7m kwa klabu ya Stoke kwa ajili ya kumsajili kiungo wa ulinzi Mfaransa Stephen Nzonzi.Hili ni ofa ya pili kutumwa kwa ajili ya kiungo huyo kwani mapema wiki iliyopita Stoke City iliitupilia mbali ofa ya £3m toka klabu ya Sevilla ya Hispania.






    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:DE GEA AIPIGA BEI NYUMBA YAKE TAYARI KUTIMKA,MOURINHO AKOMAA NA BABA RAHMAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top