AZAM FC imezibwaga klabu kongwe nchini Simba na Yanga kwa ubora wa klabu barani Afrika katika orodha iliyotolewa na mtandao wa FootballDatabase.
Katika orodha
hiyo inayofungwa na Indeni FC ya Zambia iliyoshika mkia kwenye nafasi ya 431 ya klabu zenye sifa ya kushindanishwa kwa ubora Afrika, Azam FC ndiyo inaoongoza Tanzania ikiwa nafasi ya 324 barani.
Simba inakamata nafasi ya pili nchini ikiwa nafasi ya 332 barani Afrika wakati Yanga haimo hata kwenye orodha kutokana na kukosa sifa za kushindanishwa.
5 BORA
Mabingwa wa Afrika, klabu ya TP Mazembe ya DRC wanakocheza Watanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu inaongoza bara la Afrika ikifuatwa na El Marreikh (Sudan), Vita Club (Congo), Al-Hilal Omdurman (Sudan) na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini inayokamilisha tano bora barani.
Mabingwa wa Ligi Kuu ya Kenya, Gor Mahia FC wameungana na Yanga kukosa sifa ya kuwamo katika orodha ya klabu hizo 431 zinazostahili kushindanishwa kwa ubora wa soka.
Klabu ya Zesco United ya Zambia anayoichezea mshambuliaji Mtanzania Juma Luizio, imefanya vizuri katika ubora huo na kukamata nafasi ya 133.
0 comments:
Post a Comment