728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 29, 2015

    USAJILI:CITY NAYO YAMTAKA RAMOS,LACAZETTI BEI CHINI

                               Tokeo la picha la alexandre lacazette
    Ramos:Mbio za kumsaka mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos zimeendelea kupamba moto baada ya klabu ya Manchester City nayo kuripotiwa kuingilia kati mbio hizo.Ili kumpata Ramos Manchester City italazimika kutoa
    kitita cha £63m ambacho Real Madrid mapema wiki iliyopita iliiambia Manchester United

    Imbula:Kiungo wa Marseille Gianelli Imbula 22 ameachana na mpango wa kujiunga na Inter Milan kwa mkopo na badala yake atajiunga na Porto imbayo italipa itatoa kitita cha £17.5m kama ada ya uhamisho.(L'Equipe)

    Mustafi:Real Madrid imeanza kumfuatilia mlinzi wa Valencia Shkodran Mustafi kama mbadala wa Sergio Ramos  anayetaka kutimkia Manchester United.Akiongea na kituo cha Sport 1 Kujtim Mustafi baba mzazi wa Shkrodan amesema Real Madrid wamefanya naye mawasiliano kwa njia ya simu kuhusu mwanae.

    Biglia:Real Madrid imetuma ofa ya €22m kwenda Lazio kwa ajili ya kumsajili kiungo Muargentina Lucas Biglia,27.Taarifa kutoka Italia zinasema Lazio iko tayari kumuachia kiungo huyo kwa kitita cha €30m.(La Gazzetta dello Sport)

    Fabinho:Manchester City inakaribia kufikia makubaliano ya kumsajili mlinzi mahiri wa kulia wa AS Monaco Mbrazil Fabinho,20 mwenye thamani ya £20m. (L’Equipe)

    Gervinho:Ndoto za winga wa Roma Gervinho kutimkia katika klabu ya Al Jazira ya falme za kiarabu imeota mbawa baada ya kushindwa kufikia makubaliano juu ya mshahara.Al Jazira ilitaka kumpa Gervinho mshahara wa £85,000 kwa wiki lakini nyota huyo raia wa Ivory Coast alitaka zaidi hali iliyofanya maafisa wa Al Jazira kuamua kuachana na mpango huo.

    Jovetic:Roma imejikuta katika upinzani mzito baada ya vilabu vya Juventus,Inter Milan navyo kuingia katika mbio za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Manchester City Stefan Jovetic.Jovetic,25 anataka kuondoka Manchester City baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha kocha Manuel Pellegrini.

    Lacazetti:Mshambuliaji Alexander Lacazetti 23 huenda akapata mnunuzi mapema baada ya klabu yake ya Lyon kuripotiwa kupunguza bei toka £35m mpaka £21m.Lyon imefikia hatua hiyo ya kushusha bei baada ya kukumbwa na ukata mkali wa fedha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:CITY NAYO YAMTAKA RAMOS,LACAZETTI BEI CHINI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top