728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 20, 2015

    KONDOGBIA SASA NI MALI YA INTER MILAN


    Kiungo wa Monaco Geoffrey Kondogbia ameripotiwa kuwa mbioni kumwaga wino wa kuichezea klabu ya Inter Milan ya Italia kwa uhamisho wa £22m.

    Kondogbia m
    wenye umri wa 22 anatarajiwa kutua katika jiji la Milan siku ya jumatatu kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano wa kuwachezea mabingwa hao wa zamani wa ligi ya Seria A wanaojipanga kurejesha makali yao ya zamani.

    Inter imeshinda mbio hizo za kumnasa Kondogbia baada ya jana ijumaa maafisa wake wa juu kutua Monte Carlo nyumbani kwa klabu ya Monaco na kuweka mambo sawa.

    Habari hizi ni mbaya kwa vilabu vya Arsenal na Ac Milan ambavyo kwa kipindi kirefu vimekuwa vikihusishwa na mpango wa kumsajili nyota huyo wa nafasi ya kiungo cha ulinzi.
    (Chanzo:SkySports)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KONDOGBIA SASA NI MALI YA INTER MILAN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top