WACHEZAJI wapya wa kigeni wa Yanga SC, beki Joseph Tetteh Zutah kutoka Ghana na mshambuliaji wa Zimbabwe, Donald Ngoma wamesaini Mkataba wa miaka miwili kila mmoja leo kuichezea klabu hiyo.
Katibu wa Yanga SC, Dk Jonas Tiboroha amesema kwamba wawili hao waliowasili Dar es Salaam Jumamosi asubuhi wamesaini Mikataba hiyo leo makao makuu ya klabu,Jangwani, Dar es Salaam.
“Kwa kweli tumefurahi kukamilisha zoezi hili leo. Ni hatua moja katika kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao,”amesema Tiboroha
0 comments:
Post a Comment