Santiago,Chile.
Kile kitendawili cha wapi kiungo wa klabu ya Juventus Arturo Vidal atakuwa msimu ujao huenda kikapata jibu mara baada ya michuano ya Copa America kufikia tamati yake wiki ijayo.
Gazeti la maa
rufu la michezo la Chile,La Stampa ambalo ndilo lilikuwa la kwanza kuripoti kuwa winga Alex Sanchez amesaini Arsenal mapema jana rimeripoti kuwa klabu ya Juventus ilishakubali kitita cha £21m toka klabu ya Arsenal kwa ajili ya kiungo huyo kipenzi cha mashabiki wa jiji la Torino.
La Stampa limeendelea kuripoti kuwa hatima ya Vidal ilishafikiwa mara baada ya Juventus kumsajili kiungo Sami Khedira toka Real Madrid kwa uhamisho huru.
0 comments:
Post a Comment