728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 17, 2015

    KUTIMULIWA KWA JERRY MURO,YANGA YAFUNGUKA

                                         
    Kufuatia taarifa kuzagaa mtaani kwamba,Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amefutiwa kibarua chake kwenye klabu hiyo ya Jangwani,
    uongozi wa
    timu hiyo umeamua kulitolea ufafanuzi jambo hilo ili kuondoa utata na maswali mengi yanayoulizwa na mashabiki wa mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu uliopita.

    Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha amesema, hakuna ukweli wowote juu ya jambo hilo na kuongeza kuwa Jerry Muro bado ni Afisa habari wa Yanga na ni mfanyakazi halali wa klabu hiyo na hakuna kikao kilichoitishwa kuchukua uamuzi huo.

    “Hakuna ukweli juu ya jambo hilo, Jerry bado ni afisa wa habari na mahusiano na ni mfanyakazi wa Yanga, na hicho kikao sidhani kama kilifanyika maana mimi ndiye ninayeitisha vikao na si
    jaitasha kikao cha hivyo”, amesema.
    “Nimeshangaa hata mimi kwasababu nimeona kwenye ‘groups za WhatsApp’ jana.Nimeshawahi kuongea wakati mwingine unakuta taarifa zimeandikwa kwenye blogs,sasa sijui huyu mtu aliyeandika yeye taarifa anazitoa wapi”, alifafanua.

    “Mashabiki wa Yanga waelewe kwamba, Jerry Muro bado ni mtumishi wa Yanga na bado ataendelea kuwahabarisha habari za Yanga.

    Tunajaribu kuangalia na kuchunguza chanzo cha hiyo habari ni nini”, Tiboroha alimaliza.Awali,kulikuwepo na taarifa zilizo zagaa kwenye mitandao ya kijamii (social networks) kwamba afisa habari wa Yanga Jerry Muro ametimuliwa kunako klabu hiyo lakini habari hizo hazikwenda ndani zaidi kueleza sababu zilizopelekea Yanga kumtimua Muro

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KUTIMULIWA KWA JERRY MURO,YANGA YAFUNGUKA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top