Habari na Paul Manjale.
ABRAMOVIC v MOURINHO
Wakati kocha Jose Mourinho akipambana usiku na mchana kuhakikisha mlinda mlango wake Peter Cech haendi Arsenal na badala yake aende mbali kabisa na ligi ya England (Epl) mmiliki wa klab
u hiyo Mrusi Roman Abramovich yeye amekuwa na mtazamo tofauti juu ya jambo hilo.
Kwa kuanzia Abramovich ameamua kuingilia kati na kusema mlinda mlango huyo mwenye miaka 33 aachwe aamuwe mwenyewe ni wapi anataka kwenda hii ni kama kulipa fadhira kwa yote yaliyofanywa na nyota huyo toka Czech.
MTONYO:£4M
Kama hiyo haitoshi Abramovich ameamua kumzawadia Cech kiasi cha £4m kitu ambacho ni kigeni katika soka na hakijawahi kufanywa kwa nyota yoyote yule katika klabu ya Chelsea na pengine katika vilabu vingine England.

Cech atapokea kiasi hicho cha pesa ikiwa ni mshahara ambao angelipwa endapo angemaliza mkataba wake uliobaki Chelsea pamoja na pesa nyingine ya ziada toka kwa mmiliki wa klabu hiyo bilionea Roman Abromovic kama asante kwa utumishi mwema.
Cech anaondoka Chelsea baada ya kuitumikia klabu hiyo ya London kwa miaka 11 ikiwa ni miezi 12 tu tangu Abromovich ainunue klabu hiyo yenye historia kubwa England mwaka 2004.
MAFANIKIO YA CECH AKIWA NA CHELSEA
Mataji manne ya ligi kuu,mataji manne ya kombe la FA,mataji matatu ya kombe la ligi (Carling/Capital One Cup),Champions ligi (1) na Europa ligi (1).
Mataji manne ya ligi kuu,mataji manne ya kombe la FA,mataji matatu ya kombe la ligi (Carling/Capital One Cup),Champions ligi (1) na Europa ligi (1).
0 comments:
Post a Comment