La Serena,Chile.
Ikishuka dimbani Estadio La Portada timu ya taifa ya Argentina imeibuka na ushindi wake wa kwanza wa michuano ya Copa America 2016 baada ya kuichabanga timu ya taifa ya Uruguay kwa goli 1-0.
Argentina iliyokuwa
imesheheni nyota wake wote ilijipatia goli hilo la pekee dakika ya 56 kwa kichwa safi cha karibu cha mshambuliaji wake Sergio Aguero akiunganisha krosi ya mlinzi wa kulia Pablo Zabareta..
Huu ni ushindi wa 82 wa Argentina dhidi ya Uruguay kati ya mara 178 walizokutana katika historia ya mataifa hayo nguli ya soka barani Amerika ya Kusini.
Katika mchezo mwingine wa kundi B,Paraguay imepata ushinda wa goli 1-0 dhidi ya wageni waalikwa Jamaica.Paraguay ilipata goli lake la pekee kupitia kwa mshambuliaji Edgar Benitez aliyetumia vyema makosa ya mlinda mlango wa Jamaica Duwayne Kerr.
Kufuatia matokeo hayo Argentina na Paraguay kwa pamoja zinaongoza kundi hilo zikiwa na alama 4 huku Uruguay ikiwa na alama 3,Jamaica inaburuza mkia yenyewe haina alama yoyote mpaka sasa.
Mechi zijazo za kundi hilo Jamaica v Argentina,Uruguay v Paraguay.
0 comments:
Post a Comment