SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania kutoka watano hadi sa
ba kuanzia msimu ujao.
Hayo yaamepitishwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya TFF kilichofanyika kuanzia Saa 3:00 asubuhi hadi Saa 11:30, ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo, eneo la Kikwajuni, Zanziba.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichoongozwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi zimesema kwamba pamoja na hayo,kila klabu italazimika kumlipia kila mchezaji ada ya dola za Kimarekani 2,000 (Sh. Milioni4) kwa msimu.
0 comments:
Post a Comment