728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 28, 2015

    ONGEZEKO LA WAGENI:MALINZI AFUNGA RASMI MJADALA NA VILABU

    Dar es Salaam.

    Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema kama klabu zinaona kuwa wachezaji saba wa kigeni hawatoshi, zinaweza kusubiri na kuendelea na mjadala huo na mwakani jambo hilo litaanga
    liwa upya.

    Yanga, Azam na Simba zilipeleka maombi TFF kuitaka iongeze wachezaji kutoka watano waliopo hadi 10 ili wazisaidie hasa katika michezo ya kimataifa.
    Licha ya TFF kuongeza idadi mpaka kufikia wachezaji saba, klabu zilifurahi hilo, lakini bado wameona idadi hiyo haitoshi na walipendekeza kuwa ni bora TFF ingeziacha klabu kusajili wachezaji wa kigeni idadi wanayotaka.

    “Hili suala la idadi ya wachezaji wa kigeni limeleta mjadala katika nchi nyingi duniani kwa sababu kila mmoja ana maoni yake.”

    “Mwaka jana nilifanya kikao na klabu 14 za Ligi Kuu, wenyeviti wote walikuwepo,walichoniambia achilia mbali mambo ya kuweka ukomo wa wachezaji watano,sisi tunataka idadi isiyo na kikomo, acha wenye fedha wachukue wachezaji wa nje waweke kwenye timu zao na sisi ambao hatuna fedha tutawatumia wachezaji wazawa na tutawafunga,” alisema Malinzi akikariri kauli za baadhi ya klabu.

    Aliongeza: “Licha ya kuongeza, lakini jambo hili bado lina mjadala mkubwa kwani kuna upande wanasema unapokuwa na wachezaji wengi wa nje
    unaichangamsha ligi, unawapa changamoto wachezaji wazawa, unaongeza uwezo wao wa kupambana, pia unaiuza ligi nje kwani ligi yetu inaonekana nchi nyingi, lakini upande mwingine wapo wanaodai kuwa unaiua timu ya Taifa, hivyo ni mjadala mpana,” alisema.

    “Kanuni za Ligi Kuu siyo msahafu, ni kitu ambacho kinaandaliwa na kamati ya utendaji ambao nao ni binadamu, mimi naomba huu mjadala uendelee mwakani tutatunga tena kanuni ikiwezekana kubadilisha tutabadilisha,” alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: ONGEZEKO LA WAGENI:MALINZI AFUNGA RASMI MJADALA NA VILABU Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top