London,England.
Mlinda mlango Peter Cech,33 amefaulu vipimo vyake vya afya alivyofanya jana ijumaa katika klabu ya Arsenal.
Cech aliwa
sili jana katika viunga vya makao makuu ya klabu ya Arsenal na kufanyiwa vipimo ili kujua utimamu wa afya yake kabla ya kusaini mkataba utakao muwezesha kuingia katika vitabu vya historia vya Arsenal kwa kuwa mlinda mlango anayelipwa mshahara mkubwa zaidi.Cech atakuwa akilipwa mshahara wa £100,000 kwa wiki ambao ni sawa na ule aliyokuwa akilipwa katika klabu ya Chelsea.
Habari za kuaminika toka vyanzo vya karibu ni kwamba Peter Cech atatangazwa jumatatu ijayo kuwa mchezaji mpya wa Arsenal na kuhitimisha safari ya miaka 11ya mafanikio makubwa akiwa na klabu ya Chelsea.
Wakati huo huo kocha wa makipa wa Chelsea Christoph Lollichon ambaye anahusishwa kumfuata Cech katika klabu ya Arsenal amesema hana uhakika kama uongozi wa klabu hiyo utamruhusu kuhama hii ni kutokana na ugumu aliouona katika suala la uhamisho wa Peter Cech.
0 comments:
Post a Comment