Jara:Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Mainz Christian Heidel amesema klabu hiyo imemuweka sokoni nyota wake Mchile Gonzalo Jara baada kufadhaishwa na kitendo cha kihuni alichomfanyia mshambuliaji wa Uruguay Edinson
Cavani katika michuano inayoendelea ya Copa America na kumsababishia kadi nyekundu.
Payet:Klabu ya West Ham United leo mchana itatangaza kumsajili kiungo wa klabu ya Marseille Dimitri Payet,28 baada ya nyota huyo mapema jana kifaulu vipimo vya afya yake.
Turan:Mgombea uraisi wa klabu ya Barcelona Josep Maria Bartomeu,52 ameahidi kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Arda Turan mwenye thamani ya €14m ikiwa atachaguliwa kuiongoza klabu hiyo kwa mara ya pili.
Vidal:Gazeti la Marca limeripoti kuwa klabu ya Juventus tayari imeshamuuza siku nyingi kiungo wake mahiri Arturo Vidal kwa klabu moja kubwa kinachosubiriwa ni kuisha kwa michuano ya Copa America ndipo taarifa rasmi itolewe.
Abdennour:Klabu ya Newcastle imetuma ofa ya £12m katika klabu ya Monaco kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kati Mtunisia Aymen Abdennour.Mlinzi huyo mwenye miaka 26 ataruhusiwa kuondoka Monaco ikiwa dau la £15m litawekwa mezani kwa ajili yake.
Schneiderlin:Klabu ya Manchester United huenda wiki ijayo ikafanikiwa kutangaza kumsajili kiungo wa klabu ya Southampton Mfaransa Morgan Schneiderlin baada ya kuripotiwa kukubali kutoa dau la £24m.(Mirror)
Paulinho:Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs Mbrazil Paulinho huenda akatua katika klabu ya Guanhzou Evergrande inayokipiga katika ligi ya China.Paulinho anawindwa na miamba hiyo ya Asia inayofundishwa na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Felipe Scolari baada ya kukosa namba katika kikosi cha Tottenham hasa baada ya ujio wa kocha Mauricio Pochetino.
Ghoulam:Klabu ya Arsenal inajiandaa kutuma ofa ya £11m kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa kushoto wa klabu ya Napoli Faouzi Ghoulam,24.Habari za kuaminika zinadai kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ni shabiki namba moja wa mlinzi huyo raia wa Algeria.
Kovacic:Klabu ya Barcelona imeripotiwa kuingia katika mbio za kumsaka kiungo wa klabu ya Inter Milan Mateo Kovacic,21 anayewinda kwa udi na uvumba na klabu ya Liverpool.Ili kufanikisha usajili huo Barcelona iko tayari kuwatoa Alex Song na Martin Montoya kama chambo cha kumnasa kiungo huyo MCroatia.
Cech:Mlinda mlango Peter Cech leo ijumaa anatarajiwa kuwasili katika makao makuu ya klabu ya Arsenal tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea klabu hiyo ya kuskazini mwa jiji la London mapema wiki ijayo.(BBC)
0 comments:
Post a Comment