728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 22, 2015

    YANGA YAMGOMEA KOCHA WAKE KUINOA STARS

     
    KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imewekewa ngumu na Klabu ya Yanga, baada ya Wanajangwani hao kumgomea kocha wao kuifundisha Taifa Stars.

    Juzi kamati hiyo ilimtimua aliyekuwa Kocha Mkuu wa Stars, Mart Nooij, baada ya kulala kwa mabao 3-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Uganda kwenye mchezo wa kufuzu Kombe la Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (Chan) uliopigwa kwenye Uwanja
    wa Amaan mjini Zanzibar.

    Mara baada ya mchezo huo, kamati hiyo ilikubaliana kumpa timu hiyo mzalendo Charles Boniface Mkwassa, ambaye ni kocha msaidizi wa Yanga na aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Zanzibar, Hemed Morocco, lakini Yanga wamemgomea kocha wao kuifundisha Stars.

    Chanzo cha ndani kimelieleza kuwa mara baada ya Mkwasa kupigiwa simu na kupewa dili hilo, aliomba kuzungumza na waajiri wake wa sasa, lakini baadaye alirudisha jibu kuwa wamemkatalia wakidai kama ni fedha watamuongezea.

    “Aliomba kuzungumza na waajiri wake ambao ni Yanga, lakini waligoma, hata viongozi wa kamati ya utendaji waliwasiliana na viongozi wa Yanga, lakini wakaweka ngumu kumuachia kocha huyo.
    “Kwa Tanzania kwa sasa tunaona huyu ndiye kocha anayeweza kuisaidia timu hii ikafika mbali, unajua huyu ana leseni A ya Caf, Morocco naye ana leseni A, kwa hiyo ni makocha wasomi.

    “Bado hatujakata tamaa, tunaamini wanaweza kukubali ingawa hali inaonekana kuwa ngumu.
    “Morocco yeye hana shida atatua Dar es Salaam kesho (leo) kwa ajili ya kuanza majukumu yake,” kilisema chanzo hicho.Kazi ya kwanza ambayo makocha hao watatakiwa kuifanya ni kuhakikisha wanaivusha Stars kwenye
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA YAMGOMEA KOCHA WAKE KUINOA STARS Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top