Parma,Italia.
Klabu ya Parma ya Italia rasmi leo imetangazwa kufilisika na hatimaye kushushwa daraja mpaka ligi ya ridhaa daraja la nne (Seria D) tena ikiwa
na jina jipya baada ya kushindwa kupata mnunuzi mpaka siku ya mwisho ya kujisajili kwa ajili ya ligi ya Seria B ambayo ni jumatatu ya leo juni 22 mchana.
MSIMU ULIOPITA
Mwezi machi 2015,Parma ilitangaza kufilisika huku ikiwa na deni la €200m ($220m) huku ikiuzwa mara mbili ili kuinusuru kiuchumi lakini bado hali ilikuwa mbaya kiasi cha kufanya michezo yake miwili ya Seria A kuahirishwa kutokana na kukosa fedha za kujikimu.
YACHEMKA DAKIKA ZA MWISHO!!
Ndoto za Parma kucheza ligi daraja la pili (Seria B) zilizimika ghafla baada ya wanunuzi kujitoa dakika za mwisho kabisa siku ya jana jumapili.Wanunuzi hao walikuwa ni Giuseppe Corrado na Mike Piazza.
KUFULIA
Je,Parma ndiyo klabu ya kwanza kukutwa na kadhia hiyo katika ligi ya Seria A?
Hapana!!Vilabu vya Fiorentina na Napoli navyo vilishawahi kukumbwa na kadhia hiyo lakini baada ya muda vikaibuka tena na kuendelea kuyatumia majina yao ya zamani.
KUBADILI JINA
Je,ni lazima kubadilisha majina?
Kubadilisha majina na lazima ukikumbwa na kadhia kama hii ya kushushwa mpaka Seria D kwani ligi hii inakuwa na sheria na taratibu zake.Parma wanaweza kuitwa Parma tena iwapo watajijenga kiuchumi na kurejea juu vinginevyo huu utakuwa ndiyo mwisho wao.
MAFANIKIO
Parma iliwahi kutwaa vikombe vikubwa vya Ulaya miaka ya 1990's,UEFA CUPS (2) na Kombe la Washindi (1)
0 comments:
Post a Comment