728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, June 28, 2015

    USAJILI:CILLESSEN KUMRITHI DE GEA MAN UNITED,BEI YA SERGIO RAMOS KIBOKO


    Augustinsson:Klabu ya Liverpool iko katika mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa kikosi cha Sweden cha U-21,Ludwig Augustinsson
    anayechezea klabu ya FC Copenhagen.(Daily Mirror)

    Di Maria:Manchester United iko tayari kumtoa winga wake Angel Di Maria kwenda Paris St-Germain kwa ajili ya kumpata mshambuliaji wa miamba hiyo ya Ufaransa Edinson Cavani.(Daily Star)

    Ramos:Real Madrid imeiambia Manchester United kutoa £63m kama kweli inataka kumsajili mlinzi wake mahiri Sergio Ramos.(Sunday People)

    Cillessen:Manchester United imeripotiwa kutenga kitita cha £20m kwa ajili ya kumsajili mlinda mlango wa klabu ya Ajax Mdachi Jasper Cillessen kwa ajili ya kuchukua nafasi ya David De Gea anayewindwa kwa nguvu zote na Real Madrid.(Daily Mirror)

    Vidal:Juventus imeripotiwa kukubali kumuuza kiungo wake Arturo Vidal,28 kwenda Arsenal kwa ada ya £21m na tayari mkataba wa miaka mitano umeshaandaliwa kwa ajili ya kiungo huyo mpambanaji.(Metro)

    Ba:Shanghai Shenhua kupitia mtandao wake imedai kumsajili mshambuliaji wa Besiktas Msenegal Demba Ba kwa kitita cha £9m.(Sunday Express)

    Schneiderlin:Southampton imeanza kujiandaa na maisha bila ya kiungo wake Morgan Schneiderlin baada ya kuripotiwa kuanza kuwafukuzia viungo Jordy Clasie na Idrissa Gueye.(Sunday Express)

    Pogba:Manchester City imesema iko tayari kumnunua Paul Pogba kwa kutoa ada ya  £71m inayotakiwa na Juventus ikiwa kiungo huyo ataiomba klabu hiyo ya Italia ruhusa ya kuhama.(Sunday Mirror)

    Ogbonna:West Ham imeipiku usukani Everton katika mbio za kuisaka saini ya mlinzi wa Juventus Angelo Ogbonna baada ya kuripotiwa kuwa tayari kufikia bei inayotakiwa na Juventus ya £12m.(Sunday Mirror)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:CILLESSEN KUMRITHI DE GEA MAN UNITED,BEI YA SERGIO RAMOS KIBOKO Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top