728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, June 20, 2015

    STARS YATIA AIBU TENA,YADUNDWA 3-0 NA UGANDA NYUMBANI

    Zanzibar.


    Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars" leo tena imeendelea kuwahudhunisha  Watanzania baada ya kupokea kipigo cha magoli 3-0 toka kwa timu
    ya taifa ya Uganda katika kinyang'anyiro cha kusaka tikeki ya kushiriki michuano ya wachezaji wanaocheza soka la ndani maarufu kama Chan.

    Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Amaan Zanzibar leo usiku,Stars ilishindwa kuwamudu vijana wa Uganda ambao tangu mwanzo wa mchezo walionyesha kuwa wamekuja kusaka ushindi na siyo vinginevyo.

    Kufuatia kipigo hicho Stars imejiweka katika mazingira magumu ya kufuzu Chan kwani ili isonge mbele italazimika kuifunga Uganda jumla ya magoli 4-0 ugenini kitu ambacho ni kigumu sana.

    NOOIJ CHINI YA ULINZI
    Kama kuna mtu aliyekuwa na wakati mgumu pengine kuliko wote katika mchezo huo basi ni kocha wa Stars Mart Nooij ambaye baada ya kipenga cha mwisho ilibidi atoke uwanjani akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi kuhofia mashabiki wenye hasira.

    WACHEZAJI WAKOSA DONGE NONO
    Wachezaji wa Stars wamekosa donge nono la shilingi milioni moja moja (1,000,000) waliloahidiwa na TFF kupata iwapo wangeifunga Uganda (The Cranes) katika mchezo wa leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STARS YATIA AIBU TENA,YADUNDWA 3-0 NA UGANDA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top