728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 26, 2015

    MZUNGU WA SIMBA ATUA DAR TAYARI KUANZA KAZI

    Kocha mpya wa Simba, Dylan Kerr ametua leo mchana jijini Dar es salaam tayari kuanza kazi ya kuiandaa timu kwa ajili ya ligi kuu soka Tanzania bara.

    Kerr, raia wa Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.

     Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na  South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini.

    Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MZUNGU WA SIMBA ATUA DAR TAYARI KUANZA KAZI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top