Klabu ya Swansea City imeendelea kujizatiti kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu ya England baada ya leo hii kukamilisha usajili wa mlinzi wa Saint-Etienne ya Ufaransa Franck Tabanou.
Tabanou 26 anayeimudu vyema nafasi ya ulinzi wa kushoto na winga amesaini mkataba wa miaka mitatu ya kuichezea Swansea City baada ya klabu hiyo kuilipa Saint Etienne ada ya £3.5m.
Tabanou anakuwa mchezaji wa pili kutua Swansea baada ya kiungo Andre Ayew kutua klabuni hapo akitokea Marseille mapema wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment