728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 18, 2015

    CAF YAMPIGA ‘STOP’ NGASSA KUICHEZEA TAIFA STARS KISA KUSAINI FREE STATE

                                                   Tokeo la picha la MRISHO NGASA
    SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limemzuia kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mrisho Khalfan Ngassa kuicheze timu ya taifa, Taifa Stars dhidi ya Uganda Jumamosi.

    CAF imeiambia TFF (Shirikisho la Soka
    Tanzania) kwamba Ngassa haruhusiwi tena kucheza michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), kwa sababu siyo tena mchezaji wa Ligi ya nchini mwake.

    Ngassa aliyesaini Mkataba wa miaka minne na Free State Stars ya Afrika Kusini Mei mwaka huu akitokea Yanga SC ya Tanzania kwa sababu hiyo ameondolewa kikosini.
    Taifa Stars inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania kufuzu kwa CHAN 2016.

    Msafara wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhid ya Uganda utachezwa katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2 usiku.
    Stars inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika uwanja wa Namboole jijini Kampala.

    Mara baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.

    Kocha mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi hii.
    Wachezaji waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish, Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris na Nadir Haroub.

    Wengine ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo, Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.

    Waaamuzi wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: CAF YAMPIGA ‘STOP’ NGASSA KUICHEZEA TAIFA STARS KISA KUSAINI FREE STATE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top