Sikuwahi kufikiria kama ingekuja kutokea siku moja nitakuja kusema kwaheri kwenye klabu ya Chelsea. Klabu ambayo ilikuwa moyoni kila sekunde tangu nilipojiunga nayo Julai 2004,timu ambayo nifikiri siku moja ningetukika glovu na viatu vyangu na kumaliza safari
yangu ya soka nikiitumikia.
Lakini mara zote maisha hayako kama unavyofikiria.Tangu 2004 imekuwa ni safari ya aina yake yenye mafanikio kuliko changamoto, tumeweza kushinda kila aina ya taji lililopo kenye ligi ya England hali kadhalika yale ya Ulaya na lile kubwa kuliko la vilabu bingwa barani Ulaya.
Nikitazama nyuma kwenye mafanikio pamoja na msimu wa 2010, nyuma zaidi kwenye mataji ya 2005 na 2006,ushindi wa vikombe viwili cha EPL na FA najivunia sana hilo.
Pamoja kama timu tuliandika historia.Majira ya kiangazi ya msimu uliopita, mambo yalibadilika na nikaelewa sikuwa tena chaguo la kwanza kwenye nafasi ya golikipa lakini nikahisi haikuwa muda muafaka wa mimi kuondoka.
Wakati ligi inaendelea ilidhihirika wazi kwamba, hali yangu haingeweza kubadilika na hapo ndipo ninaamini kwa
kiwango changu sio mtu wa kuendelea kukaa benchi. Nikafanya maamuzi ya kuondoka kwenda sehemu nyingine kutafuta changamoto mpya.Kukosa nafasi ya kucheza kulinipa nafasi ya kutuliza akili yangu na kulinifanya nitambue ni kwa kiasi gani nilikuwa nikifurahia kucheza soka kwa
kiwango cha juu, kwasababu nafasi hiyo niliikumbuka mno kila mechi ambayo sikupangwa.
Nimejitoa kwenye mchezo wa soka na nina njaa ya mafanikiokama ilivyokua tangu mwanzo na ninapenda changamoto zinazoletwa na wachezaji wengine wenye viwango vya hali ya juu ninaokutana nao kwenye Premier League ligi bora na yennye ushindani wa hali ya juu duniani.
Ndio maana niliongea na Bwana Abramovich kuhusu mimi kuendelea kubakia kwenye ligi hii na ninapenda kumshuku toka kwenye uvungu wa moyo wangu kwa ushirikiano alionipa juu ya jambo hili. Inamaana sana kwangu kwasababu bila yeye klabu ya Chelsea isingefika ilipo sasa.
Anastahili pongezi nyingi kwa kile alichoifanyia klabu na sisi sote kwa ujumla .Ninamshukuru kila mmoja anayehusika na klabu ya Chelsea kwa ushirikiano wake,wachezaji, uongozi, benchi zima la ufundi na makocha wote ambao nilifanyanao kazi kwa
miaka yote.
Bila wao isingewezekana kwetu sote kufikia mafanikio hayo.Lakini shukrani za dhati ziwaendee mashabiki wote wa Chelsea.Nilifanya kilakitu kwa ajili yenu na ninyi mlirudisha upendo wenu kwangu. Sitosahau kitu hicho kamwe. Kita kaa ndani yangu milele.
Tutakutana tena lakini kwa wakati huu nitasimama kwenye goli lingiine.Ninahakika mtaikumbuka historia na kuelewa ni muda sasa wa mimi kuanza maisha mapya.Ninamtakia kilalakheri kila mmoja kwenye klabu ya Chelsea na nawatakia
kilalakheri kwenye msimu mpya ujao na baadae. Asanteni sana kwa miaka 11 ya miujiza.Petr Cech.
0 comments:
Post a Comment