728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 18, 2015

    USAJILI:LUKAKU AIBUKIA MANCHESTER UNITED,TEVEZ-NARUDI BOCA JUNIOR

    Habari na Paul Manjale:
                           Romelu Lukaku: A United target?

    Lukaku:Klabu ya Manchester United itamsajili mshambuliaji wa Everton Romelu Lukaku ikiwa itashindwa kumsajili mshambuliaji Mario Mandzukic wa klabu ya Atletico Madrid.Lukaku aliifungia Everton jumla ya magoli 20 katika msimu uliopita wa ligi.(The Sun)

    Cabaye:Klabu ya Tottenham imeripotiwa kuanza mbio za kuisaka saini ya kiungo Yohan Cabaye wa klabu ya Paris St-Germain.Mbali ya Tottenham klabu nyingine inayosemekana kuiwinda saini ya mkali huyo mwenye miaka 29 ni klabu ya Crystal Palace inayonolewa na kocha wake wa zamani katika klabu ya Newcastle United.(The Times)
    Teves:Mshambuliaji Carlos Tevez ameiambia klabu yake ya Juventus kuwa anataka kutimka klabuni hapo na kurudi nyumbani kwao Argentina kujiunga na klabu yake ya zamani ya Boca Juniors.
    Clyne:Klabu ya Southampton imeripotiwa kuanza kujiandaa na maisha mapya bila ya mlinzi wake mahiri wa kulia Nathaniel Clyne hii ni baada ya klabu hiyo kuripotiwa kuwa katika mpango kabambe wa kumsajili mlinzi Cedric Soares anayeichezea klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno.Clyne anawindwa na vilabu vya Liverpool pamoja na Manchester United.
    Shelvey:Klabu ya Tottenham imemuongeza katika usajili wake kiungo wa klabu ya Swansea City Jonjo Shelvey.Tottenham itamgeukia kiungo huyo mara tu baada ya kukamilisha usajili wa mlinzi wa Burnley Kieran Trippier.
    De Bruyne:Ndoto za klabu ya Manchester City kumsajili kiungo Kevin De Bruyne huenda zikafanikiwa baada ya taarifa kutoka Ujerumani kusema kuwa mazungumzo ya mkataba mpya kati ya kiungo huyo na klabu yake ya Wolfsburg kuvunjika.
    Fabinho:Klabu ya Monaco imeiambia klabu ya  Manchester United kutoa kitita cha £20m kama kweli ina nia ya dhati ya kumnasa mlinzi wa kulia wa klabu hiyo Fabinho.
    Schneiderlin:Klabu ya Southampton imetangaza bei rasmi ya kiungo wake Morgan Schneiderlin kuwa ni £24m.Hii ni salamu kwa vilabu vya Manchester United na Arsenal ambavyo kwa muda sasa vimekuwa vikiiwania saini ya kiungo huyo mahiri wa ulinzi.
    Rahman:Klabu ya Chelsea imeripotiwa kuwa katika mawindo wa kutaka kumsajili nyota wa klabu ya Ausburg Abdul Baba Rahman mwenye thamani ya £15m.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:LUKAKU AIBUKIA MANCHESTER UNITED,TEVEZ-NARUDI BOCA JUNIOR Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top