Saa chache baada ya kukamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Arsenal, mlinda mlango kutoka Jamuhuri ya Czech, Petr Cech amepokea vitisho kutoka kwa mashabiki wanaodhaniwa ni wa klabu ya Chelsea.
Cech, amepokea vitisho hivyo kwa njia ya ujumbe ulioandikwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo mashabiki hao walimtusi na kumtaka aiage familia yake mapema kwani muda si mrefu atapumzika kwa amani.
Mashabiki hao pia wameweka picha kwenye mitandao ya kijamii inayomuonyesha kipa huyo mwenye umri wa miaka 33, akiwa katika sura ya nyoka, hali ambayo inaashiria ni msaliti kufuatia kitendo chake cha kuihama Chelsea na kukubali kujiunga na Arsenal yenye mskani mjini London.
Petr Cech, alikamilisha mpango wa kujiunga na klabu ya Arsenal jana jioni kwa ada ya uhamisho wa paund million 10 na kusaini mkataba wa miaka minne.
0 comments:
Post a Comment