728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 18, 2015

    MAMBO YAMDODEA JAJA,AAMUA KUREJEA YANGA

                                                        
    Baada ya taarifa kusambaa kwamba mshambuliaji wa Yanga aliyetoroka, Mbrazil,Geinlson Santos Santana ‘Jaja’ anataka kurejea klabuni hapo kutokana na kushindwa kulipa fedha za kuvunja mkataba,Wanajangwani wamesema
    huo ni uamuzi wake.

    Katibu mkuu wa Yanga, Dkt. Jonas Tiboroha amesema kwamba Jaja alisaini mkataba,lakini alitoroka na wakaona njia nzuri ni kumshitaki mahakamani kwasababu Tanzania sio shamba la bibi ambapo unakuja kuvuna pesa, halafu unaondoka.

    Inaelezwa kwamba Jaja ameiambia Yanga kwamba fedha wanazotaka alipe ni nyingi mno, hivyo anaona bora arudi kuitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.
    ‘Huo ni uamuzi wake, Jaja alitolewa katika mazingira yasiyoeleweka, alisaini mkatata,lakini akatoroka, hatuwezi kupoteza fedha zetu nyingi kiasi kile, unajua wachezaji wa kigeni tunawalipa hela nyingi.

    Unaajiriwa,unachukua fedha, halafu unatoroka kana kwamba Tanzania ni shamba la bibi, unavuna hela na kuondoka “Yanga tunataka alipe hela zetu au aje kuitumikia klabu, bahati mbaya sana anaweza kuja na kukuta kanuni haziruhusu,atakuwa hana jinsi zaidi ya kulipa fedha”.

    Ameeleza Tiboroha.Kwasasa Yanga imeshajaza nafasi tano za wachezaji wa Kigeni ambao ni Kpah Sherman (Liberia), Andrey Coutinho (Brazil), Amisi Tambwe (Burundi), Haruna Niyonzima
    (Rwanda) na Mbuyu Twite (Rwanda), ingawa wanasubiri majibu ya mapendekezo yao waliyowasilisha TFF wakiomba idadi ya wachezaji wa kigeni iongezwa mpaka 10.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAMBO YAMDODEA JAJA,AAMUA KUREJEA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top