Habari na Paul Manjale
Imbula:Klabu ya Arsenal imefanya mawasiliano na baba mzazi wa kiungo wa Marseille Giannelli Imbula 22 kwa ajili ya kumsajili mkali huyo na nafasi ya kiungo cha ulinzi m
wenye thamani ya £15.7m.Arsenal iko tayari kumpa Imbula mshahara wa £54,000 kwa wiki kama alioahidiwa na klabu ya Inter Milan.
Wenger:Kocha wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ameripotiwa kuendelea na msako wa walinda mlango wapya licha ya kuwa karibu kuinasa saini ya mlinda mlango mkongwe wa Chelsea Peter Cech.Arsenal inatarajiwa kumuuza mlinda mlango wake David Ospina kwenda Fenerbahce huku Emilliano Martinez akienda Getafe kwa mkopo.
Bender:Kocha mpya wa klabu ya Borussian Dortmund Thomas Tuchel amesema klabu yake haina mpango wa kumuuza kiungo wake mkabaji Sven Bender licha ya kwamba klabu hiyo imeongeza wachezaji wapya katika safu ya hiyo.Bender amekuwa akiwindwa kwa kipindi kirefu na vilabu vya Arsenal na Liverpool.
Austin:Klabu ya Southampton imepeleka dau la €14m katika klabu ya QPR kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Charlie Austin,25.Mbali ya Southampton vilabu vingine vinavyoisaka saini ya mkali huyo wa magoli ni Newcastle United,Chelsea na Liverpool.
Alderweireld:Klabu ya Southampton imeripotiwa kuwa tayari kutoa kitita cha €25m ili kumsajili moja kwa moja mlinzi aliyekuwa kwa mkopo klabuni hapo kwa mkopo akitokea Atletico Madrid Toby Alderweireld.
Pogba:Gazeti za Marca limeandika kuwa klabu ya PSG inaandaa kitita cha £70m (€98m) ili kuvishinda vilabu vya Manchester City na Barcelona katika mbio za kumsajili kiungo wa Juventus Paul Pogba,22.
Benteke:Klabu ya Liverpool imewageukia washambuliaji wawili wa Amerika ya kusini Carlos Bacca na Salomon Rondon baada ya kukatishwa tamaa na bei ya £32.5m iliyowekwa na klabu ya Aston Villa kwa mshambuliaji Mbelgiji Christian Benteke,23.
Teves:Vilabu vya Juventus na Boca Juniors vinatarajia kukutana wiki kujadili uhamisho wa mshambuliaji Carlos Teves.Teves anataka kurudi Boca Juniors baada ya kuchoshwa na soka la Ulaya.(Sky Sport)
Chicharito:Mshambuliaji wa Manchester United Mmexico Javier Hernandez huenda akarudi tena Madrid lakini safari hii ni katika klabu ya Atletico Madrid ili kuziba pengo la mshambuliaji Mario Mandzukic aliyetua katika klabu ya Juventus.
0 comments:
Post a Comment