728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, June 29, 2015

    MAKALA:LIVERPOOL NA USAJILI WAKE

    Mwandishi:Wilbafos Julius

    HISTORIA ni muhimu sana katika kitu chochote. Watu wengi sana au taasisi nyingi sana huwa zinafanikiwa sasa, kutokana na historia ya mambo waliyofanya miaka ya nyuma.

    Historia inafanya
    uonekane, una uzoefu wa kufanya jambo fulani, na hivyo kuaminika kuwa hata, ukipewa nafasi tena bado utafanya vizuri sababu ya historia. Ni kweli historia ni muhimu sana, ila historia inakuwa haina maana iwapo unashindwa kuyafanya yale amabyo uliyoyafanya zamani, na kukupatia sifa na uzoefu unaokutangaza sasa.

    Liverpool ni moja ya timu ambazo bado inaendelea kutambia historia wakati kwa sasa haifanyi vizuri kabisa. Liverpool haijawahi kuchukua ubingwa wowote wa ligi kuu ya Uingereza tangu timu 22 za iliyokuwa first division ya UIngereza zilipojitenga kutoka “Football league” na kuanzisha “Premier League” msimu wa 1992/1993. Kabla ya hapo imewahi kuchukua ubingwa wa first division mara 18.

    Hii ni kusema kuwa katika vijana wa rika letu hakuna aliyewahi kuwaona Liverpool wakichukua ubingwa wa Uingereza live (labda kwa kuangalia mikanda ya video iliyorekodiwa miaka ya 1980’s).
    Mashabiki wa Liverpool wameendelea kutambia rekodi za miaka ya nyuma sana ambazo wengi wao walikuwa hawajazaliwa, na watu wengi hapa nchini walikuwa hawajaanza kufuatilia ligi za Ulaya. Wakati Liverpool wanachukua ubingwa wa Uingereza mara ya mwisho 1990, watanzania waliokuwa wanamiliki runinga hapa nchini walikuwa wanahesabika.

    nakumbuka wakati Ferguson anachukua ubingwa wa kwanza akiwa na Manchester United, aliwatambia sana mashabiki wa Liverpool, ila wao walimjibu, yeye na manchester yake wakishafikisha vikombe 18 vya Uingereza ndio arudi na kuongea chochote. Wakati Ferguson anastaafu Manchester United walikuwa wamechukua vikombe 20 vya Ligi ya uingereza (13 vikiwa ni PL chini yake Ferguson)

    Naamini kabisa wakati mashabiki wa Liverpool wanamwambia Fergie maneno walikuwa haamini kama inawezekana kwa timu yao kukaa miaka 23 bila kuchukua PL.


    Tatizo inaonekana bado itachukua miaka mingi kwa Liverpool kuja kuchukua ubingwa wa Uingereza.  Wamekuwa wakijitahidi kucheza soka la ushindani lakini wanakuwa wanakitu fulani wanakikosa na sioni kama msimu ujao watakuwa na chochote. Usajili wao mpaka sasa umekuwa hauna malengo. Mwaka jana walitumia fedha kusajili.

    Wachezaji wengi wapya walishindwa kufanya vizuri na ilionekana wazi kuwa hawakuwa makini. Mwaka huu wameamua kuja na mpango mpya ambapo wamechukua wachezaji ama kwa free au kwa wachezaji wasiojulikana. Nimekuwa nikijiuliza ni kweli Liverpool walikuwa wakimhitaji James Milner au sababu amepatikana bure? Nini nafasi yake uwanjani iwapo tayari inao Henderson na Can? Na Danny Ings je? Huyu ameonyesha uoga wa wazi wazi hasa baada ya kukataa jezi namba 7 au 8.

    Vipi kuhusu beki Joe Gomez kutoka Charlton, yuko tayari kuanza kikosi cha kwanza au ni kwa ajili ya siku zijazo? Na Roberto Firmino? Ni kweli ana thamani ya paund mil 29? Ataweza kuendana na kasi ya Ligi ya Uingereza? Je, kusajiliwa kwa Ings kunamaanisha nini kwa Borini, Baloteli na Lambert? Nini nafasi ya Sterling na Coutinho na ujio wa Firmino? Naona kama inarudi kule kule kwa kuwa na wachezaji wengi wasio kuwa na ubora.

    Naamini Rodgers ni kocha mzuri katika ufundishaji wa uwanjani ila kinachomuangusha ni namna anavyodili na usajili. Itakuwa ni jambo la ajabu iwapo hatomuuza Sterling katika dirisha hili la usajili.


    Naamini baada ya mwaka mmoja hata paund mil 20 hawezi kupata ingawa sasa hivi anakataa paund mil 40. Sterling hajaifanyia chochote Liverpool, na sijui nini hasa kinachowafanya wamlilie. Labda kama ni janja tu ya kutaka kumpandisha bei.

    Ingawa muda wa usajili bado unaendelea, sioni kama Liverpool ana nafasi yoyote ya kuingia kwenye nne bora. Na kuhusu kuchukua ubingwa ni swala la kuendelea kuota.

    Wilbafos Julius 
    June 24, 2015
    Morogoro, Tanzania
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAKALA:LIVERPOOL NA USAJILI WAKE Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top