728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, June 17, 2015

    USAJILI:BOATENG AITWA MAN UNITED,ARSENAL YAKATAA KUMTOA CHAMBERLAIN



    Chamberlain:Klabu ya Arsenal imekataa ombi la klabu ya Chelsea lililotaka kubadirisha wachezaji A
    lex Oxlade-Chamberlain  na Petr Cech.Arsenal inataka kutoa pesa badala ya kubadirishana wachezaji.(Daily Mail)

    Kondogbia:Kiungo wa Monaco Geoffrey Kondogbia amefanya mazungumzo ya ana kwa ana na kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuzungumzia masuala ya usajili.Kondogbia anawindwa na Arsenal na tayari ofa ya £18m ya awali toka kwa miamba hiyo ya London imetupwa na klabu yake ya Monaco.

    Boateng:Klabu ya Manchester United imeripotiwa kuanza kumfukuzia mlinzi wa kati wa klabu ya Bayern Muninch Jerome Boateng ili kuimarisha ukuta wake kabla ya msimu ujao wa Epl.

    Sakho:Klabu ya Newcastle United imeripotiwa kuendelea kusaka wachezaji wapya ili iweze kufanya vizuri msimu ujao.Safari hii wakali hao wa St James Park wameripotiwa kujipanga kumsajili mshambuliaji matata wa klabu ya West Ham striker Msenegal Diafra Sakho.(Daily Mail)

    Sterling:Klabu ya Liverpool imeiambia Manchester City kuwa kitita cha zaidi ya £45m ndicho kitakacho fanikisha usajili wa winga Raheem Sterling vinginevyo mpango huo hautafanikiwa. (Daily Mail)

    Austin:Kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameripotiwa kuandaa kitita cha £15m kwa ajili ya kumnasa mshambuliaji wa QPR Charlie Austin huku pia akitenga kitita cha £20m kumnasa winga wa klabu ya Arsenal Alex Oxlade Chamberlin.(The Sun)

    Gerson:Klabu ya Barcelona imefanikiwa kumsajili kinda Gerson 18 toka klabu ya Fluminese ya Brazil kwa kitita cha £3m.Gerson anayemudu nafasi ya kiungo cha kuchezesha atatua Barcelona mwezi januari pindi miamba hiyo ya La Liga itakapo maliza adhabu yake ya kutosajili.

    Podolski:Mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski yuko mbioni kutua katika klabu ya Galatasaray ya Uturuki kwa ada ya £1.4m baada ya vilabu vyote kufikia makubaliano.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: USAJILI:BOATENG AITWA MAN UNITED,ARSENAL YAKATAA KUMTOA CHAMBERLAIN Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top