Hatimaye Yanga imekubali kumuachia Kocha wake msaidizi Charles Boniface Mkwasa ainoe Taifa Stars.
Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), limekuomba Mkwasa ili kuchukua mikoba ya Mart Nooij.
Hata hivyo imeelezwa Mkwasa akisaidiana na Mohammed Morocco atakuwa ni kocha wa muda tu.
Awali Yanga ilikuwa imeweka ngumu, hata hivyo baadaye imekubali baada ya uongozi wa TFF kufanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.
Taarifa zinaeleza, itamtambulisha Mkwasa leo asubuhi kwenye mkutano mbele ya waandishi.
Morocco ambaye pia alikuwa wa kwanza kukubali wito, pia atatambulishwa hii leo.
0 comments:
Post a Comment