Kocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema akipewa nafasi ya kuinoa Taifa Stars,Watanzania wataona kazi.Julio amesema
ana imani kubwa kama atapewa nafasi hiyo akiwa na Charles Boniface Mkwasa na Ahmed Morocco.
“Hakika ninaamini tulijitakia wenyewe. Kama wananiamini wanipe mimi pamoja na Mkwasa na Morocco.“Najua kabisa Tanzania ina wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza na kuisaidia nchi.Achana na hisia kwamba Tanzania haina wachezaji,” alisema Julio.
TFF imemtimua aliyekuwa kocha wa Stars, Mart Nooij mara baada ya kikosi cha Stars kulala kwa mabao 3-0 dhidi ya Uganda,The Cranes katika uwanja wa Amaan,Zanzibar jumamosi juni 20.
0 comments:
Post a Comment