Carvalho:Kocha wa klabu ya Arsenal Mfaransa Arsene Wenger ameripotiwa kutuma ofa ya £28.5m kwenda klabu ya Sporting Lisbon kwa ajili ya kumsajili kiungo William Carval
ho (22).Wenger amepeleka dau hilo ambalo litaongezeka na kufikia £37m kutokana na maendeleo ya mchezaji huyo mahiri katika nafasi ya kiungo cha ulinzi.
Ogbonna:Vilabu ya Aston Villa na Southampton vimeripotiwa kuwa katika vita vikali vya kumuwania mlinzi wa klabu ya Juventus Angelo Ogbonna.Ogbonna (27) anataka kuondoka Juventus baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza tangu atue klabuni hapo mwaka 2013 akitokea klabu ya Torino.
Richards:Klabu ya Aston Villa imemsajili mlinzi Micah Richards kwa uhamisho huru akitokea klabu ya Manchester City.Richards (26) anatua Villa baada ya msimu uliopita kuchezea klabu ya Fiorentina kwa mkopo wa miezi sita.
Nzozi:Klabu ya Stoke City imekataa ofa ya £3m toka klabu ya Sevilla kwa ajili ya kiungo wake Steven N’Zonzi.(Telegraph)
Rabiot:Kiungo wa klabu ya Paris Saint-Germain Adrien Rabiot (20) amewasilisha ombi la kutimka klabuni hapo msimu huu kupitia kwa mama yake.Rabiot anataka kuondoka Paris Saint-Germain kutokana na kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha mabingwa hao wa Ufaransa. (The Mail)
Wilshere:Klabu ya Manchester City imesema itatoa kitita cha £40m kumnasa kiungo wa Arsenal Jack Wilshere ikiwa itashindwa kumsajili kiungo Paul Pogba wa klabu ya Juventus (Daily Star)
Sissoko:Klabu ya Liverpool imeripotiwa kukalia kiti cha uongozi mbele ya vilabu vya Arsenal na Chelsea katika mbio za kuinasa saini ya nyota wa Newcastle United Moussa Sissoko mwenye thamani ya £17m.
Sterling:Klabu ya Manchester City imeripotiwa kuandaa dau la mwisho la £45 million (€63m) kwa ajili ya winga wa Liverpool Raheem Sterling.
Ba:Klabu ya Besiktas imeimbia klabu ya Westham kuandaa kitika cha £8.5m kwa ajili ya kumsajili winga Gokhan Tore 23 na £15m kwa ajili ya mshambuliaji Demba Ba vinginevyo nyota hao wataendelea kubaki Beskitas
Martinez:Mshambuliaji Porto JacksonMartinez amesema klabu ya Arsenal bado haijamfuata na kumwambia kuwa ina nia ya kutaka kumsajili.Martinez (28) ameongeza ikiwa Arsenal itamfuata basi atajiunga nayo bila tatizo lolote.
0 comments:
Post a Comment