728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 19, 2015

    SAKATA LA KUTIMULIWA YANGA,JERRY MURO ATINGA MAHAKAMANI

    Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Yanga Jerry Muro amelishtaki gazeti lililotangaza kuwa amefutwa kazi kwenye klabu hiyo ambayo ndio mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa msimu uliopita.

    Muro amethibitisha kulipeleka mahakamani gazeti hilo na kudai fidia kutokan na upotoshaji huo uliofanyika dhidi yake.

    “Ni kweli msaidizi wangu Bw. Said Mbachiru alipeleka ‘demand’ kwenye gazeti la Uhuru la kuwataka mambo matatu, jambo la kwanza ni wao kuandika ‘story’ kwa ukubwa uleule,‘page’ ileile kukanusha kile walichokiandika.

    Hoja nyingine ni kuwataka wao wanipe kiasi cha shilingi milioni 50 kama usumbufu,halafu hoja ya tatu watoe ‘front page’ pamoja na maelezo ambayo mimi nitayathibisha kuhusu walichokiandika wao,kwahiyo niseme wazi tu kwenye hili hakuna kurudi nyuma”, amesema Muro.

    “Hiyo ni ‘demand’ ya kwanza kutoka kwa mwanasheria wangu, halafu wajiandae kupata ‘demand’ nyingine ya pili kutoka kwa mwanasheria wa Yanga. Tangu nimeingia Yanga sijawahi kupewa barua ya onyo,sijawahi kukaripiwa, sijawahi kupelekwa kwenye kamati ya nidhamu na maadili ya klabu na hakuna kitu ambacho kimewahi kufanyika dhidi yangu kikionesha mimi nimekuwa na utovu wa nidhamu”, alifafanua Muro.

    “Nataka kieleweke kitu kimoja, sisi ndani ya Yanga tunafanya kazi kama watu wamoja,familia moja, lakini huenda ikawa watu ambao hawako ndani ya uongozi wa Yanga wakawa wanakwazwa na kuumizwa na kauli zangu. Duniani huwezi ukapendwa na watu wote na huwezi ukachukiwa na watu wote.

    Sasa mimi nataka hao watu tukutane mahakamani, na nikwambie tu huyo mwandishi aliyetoa hiyo habari atakwenda kusema mahakamani na kuthibisha mtu aliyemwambia habari hizo, na hapo ndipo tutampata mchawi”, Muro alilalama.

    “Sikuzote nimekuwa nikisema sikwenda Yanga kubembeleza ajira, katibu wetu siku zote amekuwa imara akizungumza pasipo uoga, pasipo kificho, sisi hatukwenda Yanga kuganga njaa na wale ambao walikuwa wapo Yanga kuganga njaa safari yao imefika”,ameeleza.

    “Unajua kabla ya mtu kupewa uongozi inabidi kwanza apimwe akili, mimi sikurupuki na kuzungumza vitu ambavyo vinatoka kichwani mwangu, watu wanasema maneno ya Jerry makali lakini tunapokwenda kujenga mfumo huwezi kujenga mfumo kwa kuchekea watu.

    Na wale wanaoona nakurupuka tu kusema vitu ambavyo sijatumwa wakae wasubiri muda wangu wa uongozi uishe, na ndio maana sisi kwetu Yanga kwanza mtu baadae”,alimaliza.

    Awali zilizagaa habari kuwa Jerry Muro ametimuliwa na uongoi wa klabu ya Yanga na baadae taarifa hiyo ilionekana kwenye gazeti la Uhuru ikieleza habari hiyo ya kutimuliwa kwa Muro kunako klabu ya Wanajangwani

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SAKATA LA KUTIMULIWA YANGA,JERRY MURO ATINGA MAHAKAMANI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top