Podolski:Mshambuliaji wa Arsenal Lukas Podolski ameonekana katika Televisheni ya klabu ya Galatasaray akiwasili katika makao makuu ya klabu hiyo kukamilisha usajili ambao utatangazwa ndani ya masaa machach
e yajayo.Kuondoka kwa Podolski Arsenal huenda kukafuati wa na nyota kama Yaya Sanogo na Joel Campbell ambao wamedaiwa kutokuwa katika mipango ya klabu hiyo ya kaskazini mwa London.
Wenger:Kocha wa Arsenal Arsene Wenger ameripotiwa kutaka kuimarisha safu yake ya kiungo kwa kuwasajili ndugu wawili Lars Bender na Sven Bender huku akisisitiza kutojua chochote kuhusu kumsajili kiungo wa Juventus Arturo Vidal.
Gonzalez:Vilabu vya Manchester City, Chelsea,Fiorentina na Inter Milan vimeripotiwa kuanza kuifukuzia saini ya shujaa wa Paraguay katika michuano inayoendelea ya Copa America Derlis Gonzalez.Gonzales nyota wa FC Basel mwenye miaka 20 ndiye aliyeisukumiza nnje ya michuano hiyo Brazil baada ya kufunga mara mbili kupitia mikwaju ya penati (La Gazzetta dello Sport)
Marquinhos:Klabu ya Real Madrid huenda ikamsajili mlinzi wa klabu ya Paris Saint Germain Marquinhos ikiwa mlinzi wake Sergio Ramos atalazimisha kwenda Manchester United .
De Bruyne:Klabu ya Wolfsburg imezima rasmi minong'ono juu ya nyota wake Mbelgiji Kevin de Bruyne kutaka kuhama baada ya kutangaza kuwa kiungo huyo hauzwi na badala yake wanafanya mchakato wa kumboreshea maslahi ili aendelee kuwa na furaha klabuni hapo.
Dzeko:Irfan Redzepagic ambaye ni wakala wa mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Mbosnia Edin Dzeko amekanusha habari za mteja wako kuwa mbioni kutua katika klabu ya As Roma na kusisitiza kuwa nyota huyo bado anataka kubakia Etihad.
Balotelli:Klabu ya Sampdoria ya Italia kupitia kwa kocha wake Walter Zenga imekana kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli,23.
Pogba:Kutoka Italia habari zinasema kuwa klabu ya Juventus imekubali kumuuza kiungo wake Paul Pogba kwenda Barcelona kwa kitita cha £64m.Katika usajili huo ambao utakamilika majira yajayo ya kiangazi ya 2016 Barcelona itatoa kitita £57m kisha baadae itaongeza £7m.Uhamisho huo umesogezwa mbele kutokana na Barcelona kuwa bado inatumikia kifungo cha kutosajili mpaka januari mwaka 2016.
0 comments:
Post a Comment