KLABU ya Yanga inataka kuthibitisha ule usemi wake kuwa wao ni wa
kimataifa, hiyo ni kutokana na kile kinachoendelea kwa sasa katika mbio
zake za usajili ambapo baada ya kusajili wachezaji kadhaa wazawa, sasa
nguvu kubwa ni kwa wale wa kimataifa.
Taarifa ni kuwa usajili huo unaweza kufikia shilingi
milioni 900 ikiwa kila kitu kitaenda kama kilivyopangwa.Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga zimefafanua kuwa, idadi ya wachezaji waliotengewa dau hilo ni wanne ambapo wawili wanatoka Ghana, mmoja Liberia na wa mwisho ni Mzimbabwe, Donald Ngoma.
Imeelezwa kuwa Waghana hao ambao mmoja ni kiungo na mwingine mshambuliaji, tayari wamefanya mazungumzo na Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm aliyeko nchini humo kwa ajili ya mapumziko na wamekubaliana kila mmoja atasajiliwa kwa shilingi milioni 200, jumla 400.
Upande wa Mliberia ambaye naye pia ni straika, amekubaliana na dau la Sh milioni 200 kama ilivyo kwa Waghana. Wachezaji hao watatu wanatarajiwa kutua nchini na Pluijm ndani ya siku mbili hizi kuanzia kesho.
Ngoma ambaye anaichezea FC Platinum ya Zimbabwe, ametengewa zaidi ya Sh milioni 250 zikiwa ni gharama za kuvunja mkataba na fungu lake la usajili.
Wachezaji wazawa waliokamilisha usajili wa kutua Yanga ni Deus Kaseke kutoka Mbeya City, Malimi Busungu (Mgambo JKT), Benedict Tinoco (Kagera Sugar).Ikiwa Yanga itatimiza yote hayo basi itaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kusajili kwa gharama kubwa kiasi hicho.

“Tumeshafanya nao mazungumzo na mambo yamekaa vizuri, ingawa
kitatoka kiasi kikubwa cha fedha, Waghana wanaweza kuja na kocha.“Mbali
na gharama hizo za usajili, pia kuna gharama za kuwasafirisha pamoja na
huduma ndogondogo, hivyo jumla ni kama shilingi milioni 900 zinaweza
kutumika,” alisema mtoa taarifa na kuongeza:
“Lakini hata wakija hatutawasajili kwanza, tutasubiri sheria ya
wachezaji nane wa kigeni tuliyoipendekeza kuona kama itapitishwa,
ikishindikana basi tutamchukua Ngoma na Mghana mmoja.”
Wachezaji wazawa waliokamilisha usajili wa kutua Yanga ni Deus Kaseke kutoka Mbeya City, Malimi Busungu (Mgambo JKT), Benedict Tinoco (Kagera Sugar).Ikiwa Yanga itatimiza yote hayo basi itaweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kusajili kwa gharama kubwa kiasi hicho.
0 comments:
Post a Comment