728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Kocha Mayanga Nimekuelewa sana ..... Lakini

                

    Chiki Mchoma , Dar es salaam                                                    
          
    Kwenye Mapambano ya Vita baina ya nchi kwa nchi au vyovyote itakavyokuwa kuna watu maalum ambao jukumu lao ni kuongoza Mapambano hayo ili kuleta ushindi kwa Vikosi vyao vya Kijeshi. 

    Kwenye Mstari wa mbele wa Vita hutakuta Viongozi wa Ngazi za juu wa Kijeshi hata Mmoja.

    Wote wako kwenye maeneo ya Mbali wakichora ramani za Mapambano na kutumia elimu zao na uzoefu wao wa kivita kupeleka mbinu kwenye uwanja wa Mapambano. 

    Mbinu za kivita zikishakamilishwa na Majemedari hupelekwa moja kwa moja kwa Mtu Muhimu kuliko wote kwenye uwanja wa Mapambano anayeitwa 'Captain'. 

    Huyu ndiye mtu mwenye dhamana na utaalamu wa kutafsiri mbinu zilizoletwa vitani na Majemedari na kisha kuzitafsiri kwa wapiganaji na hatimaye kupata Ushindi kutokana na umakini na uhodari wa 'Captain' wao. 

    Pale Mtibwa kuanzia miaka ya mwanzoni mwa 1990 ambapo Mtibwa ilikuwa inajiimarisha kufikia Malengo yake hadi 1995 na kuendelea alikuwepo mpiganisha vita huyo aliyetafsiri vema mbinu za Jemedari Mkuu wa Kikosi cha Mtibwa Kocha John Simkoko na Kocha Msaidizi Ahmed Mumba... Huyo si Mwingine ni *'CAPTAIN SALUM MAYANGA.'*

    Kocha Mzalendo wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Salum Mayanga nimemuelewa sana na kwa sababu hiyo nampa Kongole. (Kiswahili kipya cha wataalamu wa Kiswahili chenye maana ya kumpa Mwanaume pongezi badala ya kusema neno Hongera mana inasemekana neno Hongera hupewa Mwanamke.)

    Kocha Mayanga nakupa Kongole kwa mambo kadhaa. 

    Kwanza kwa kuwa nakufahamu kwa muda mrefu haswa ulipokuwa ukiichezea Mtibwa Sugar na hasa kwa kuwa ulikuwa nahodha wa Kikosi kwa kipindi kirefu sana. 

    Jina lako halikutamba sana lakini kazi yako ilikuwa bora na makini mno kiasi kwamba katika Wachezaji wengi wenye majina waliokuwa wamekuzunguka pale Manungu... Wote walikutii na kukuita kwa jina la heshima 'Captain.'

    Kaka yangu Marehemu John Thomas Masamaki ( Huyu nilikuwa naye TPC Moshi nikimshuhudia ), Kassim Mwabuda ( Niko nae mpaka sasa Friends Veterans na bado anautwanga kweli kweli), Vincent Peter 'Mzee wa Temboni ' Kaka yangu Godfrey Karumbeta 'Fundi',Kamba Luffo 'Midfield  Kisheti' kwa kutaja Wachache.... Hawa wote walikaa kimya ulipokuwa unatoa maelekezo kwao ukiwa ndio sauti ya Kocha Simkoko uwanjani. 

    Nimetaja Wachezaji hao ambao wengi wao kwa mtazamo wangu waliwika sana kuliko wewe lakini mwisho wa siku kila walipolisikia jina lako walijua anazungumziwa Kiongozi wa Mapambano uwanjani 'Captain'.

    Sijasahau msimu uliopita ulipoirithi Prisons iliyochoka na hatimaye ukaiimarisha katika namna ambayo binafsi ni kama niliikatia Tamaa lakini katika Maajabu yako ya Ufundishaji Prisons ilimaliza katika nafasi Nne za Juu. 

    Nije Moja kwa Moja kwenye Kile ninachokupa Kongole hasa kwa Stars hii Uliyonayo na namna ninavyoiona itafanikiwa mbele yako. 

    Nimeiona Stars Mpya mikononi mwako...

    Stars ambayo angalau inaweza kupasiana mpira kwa kuguswa na Wachezaji wengi kwa uhakika. 

    Stars ambayo Wachezaji wana Ari ya Kuitumikia. 

    Stars ambayo hutumii nguvu nyingi kuielekeza. 

    Stars ambayo Wachezaji wanainjoi kuchezea mpira. 

    Stars ambayo Watanzania waniona ikiwa na mkusanyiko wa vijana wengi. 

    *Hata hivyo :*

    Sina nia ya kukusifia tu ila kukuonesha baadhi ya Mapungufu madogo lakini muhimu niliyoyaona. 

    *Kucheza na Jukwaa.*

    Waambie Vijana wako... Zipo sehemu timu itakwenda kelele za wanaowashangilia zitamezwa na wanaowazomea.... Waachane na Mpira wa Majukwaa... Wapiganie timu. 

    *Mfungaji ni Yeyote aliye kwenye Nafasi nzuri Zaidi.*

    Imejitokeza mtu analazimisha kufunga yeye wakati hayupo kwenye eneo sahihi na hayupo kwenye nafasi sahihi... Ushindi wa Timu si suala la Sifa binafsi ni Suala la 'Team Work.'

    *Kushinda Magoli Mengi ni Usalama kwa Timu.*

    Nimeshaona mara kadhaa mtu akitia Mbwembwe badala ya kuhakikisha kila nafasi ya kufunga Goli inatumiwa ipasavyo. 

    *Eneo la Ulinzi wa Kati Bado.*

    Najua hata wewe Unajua... Walinzi wetu wa Kati Bado hawana uwiano mzuri wa Maamuzi.

    *Timu zingine Zina Wachezaji Wazuri zaidi ya Hizi Tatu.*

    Hii si lawama ila ni kukukumbusha tu kuwa kama Maxio Maximo alivyopewa gari maalum ili apate fursa ya kupita kwenye kila mechi na kushuhudia uwezo wa Wachezaji mbali mbali ili kuwaita Taifa Stars... Nawe hii ni Haki yako... Waambie... Itumie. 


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kocha Mayanga Nimekuelewa sana ..... Lakini Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top