728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Yondani , Ngoma na Kamusoka ruksa kuondoka Yanga


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                         

    Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Tanzania Yanga SC inayoongoza ligi mpaka sasa Kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mahasimu wao Simba Huku kila timu ikibakiwa na mechi tano  kumalizika kwa msimu pia timu ya Yanga Na Jumamosi ya wiki Hii Itacheza mechi Play off ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger Katika uwanja wa Taifa na watarudiana wiki moja huko Algeria Pia Yanga ipo kwenye kombe la shirikisho Tanzania maarufu kama Azam Sports Federation Cup Hatua ya robo fainali ambapo watacheza dhidi ya Tz Prison April 22 uwanja wa taifa.

    Kuelekea mwisho wa msimu Uongozi wa timu ya Yanga umetoa ruhusa Kwa mchezaji yoyote kuondoka iwapo tu atafuate taratibu.Katibu wa Yanga Boniface Mkwasa Amesema 

    'Kama kuna Mchezaji anataka kuondoka basi awe muungwana, atueleze mapema na taratibu zifuatwe sisi tutamruhusu kuondoka 'Pia kama kutakuwa na mchezaji ambaye Mwalimu naona hamhitaji sisi tutafuata taratibu na kumueleza mapema kabisa Alisema Boniface Mkwasa kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania. 


    Wakati akiyasema hayo mkwasa kuna Hatari timu ya Yanga ikawakosa wachezaji wengi mhimu ambao mikataba yao inaelekea Kiisha ndani ya Yanga.  Wazimbambwe wawili Donald Ngoma na Thaban Kamusoko mwisho wa msimu mikataba yao inaisha na Uongozi wa Yanga haijaongea lolote kuhusu kuwaongezea mikataba, Pia Mabeki wa Kati wazawa Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub Cannavaro mikataba yao inafikia tamati mwisho wa msimu,  hivyo hivyo Kwa Washambuliaji wazawa Anthony Mateo na Malima Busungu.

    Pia beki wa kimataifa wa Togo Vicent Bossue na Mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi Amis Tambwe. Yanga unaweza kusema huu ndio msimu Hatari kuliko yote Kwani wachezaji wengi mikataba yao inaisha msimu huu.  Wachezaji wengine ambao  mikataba yao inafikia tamati mwisho wa msimu ni Oscar Joshua,  Hajji Mwinyi, Deusi Kaseke,  Said Juma makapu,  na Godfrey Mwashiuya. Bila kumsahau fundi wa Mpira Haruna Niyonzima.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yondani , Ngoma na Kamusoka ruksa kuondoka Yanga Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top