Mbeya,Tanzania.
LIGI KUU ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL imeendelea tena leo kwa mchezo mmoja kuchezwa huko jijini Mbeya ambapo Mbeya City walikuwa nyumbani kwenye Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine kuwaalika wakata miwa,Mtibwa Sugar kutoka Manungu,Morogoro ambapo mpaka dakika tisini zinakwisha timu hizo zimetoshana nguvu baada ya kufungana bao 1-1.
Wageni Mtibwa Sugar ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao baada ya Jaffary Salum kufunga katika dakika ya 66.Bao hilo halikudumu sana kwani dakika kumi baadae,katika dakika ya 77 Zahora Pazzi aliwafungia wenyeji Mbeya City bao la kusawazisha na kufanya mchezo huo ushindwe kumpata mbabe.
Matokeo hayo yameifanya Mbeya City ichupe mpaka nafasi ya saba baada ya kujikusanyia pointi 31.Mtibwa Sugar imebaki katika nafasi yake ya tano licha ya leo kuongeza pointi moja na kufikisha pointi 35.Timu zote zimecheza michezo 26.
0 comments:
Post a Comment