MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Saidi Mohamed Mtanda, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha linaweka utaratibu wa kuzibana klabu za soka nchinio kuhakikisha pesa zinazolipwa kwa ajili ya usajili wa wachezaji zinakatwa kodi.
Mtanda ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga
(CCM), ameyasema hayo jijini hapa leo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ipate uanachama katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
(CCM), ameyasema hayo jijini hapa leo wakati wa hafla ya maadhimisho ya miaka 50 tangu TFF ipate uanachama katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Amesema nchi hainufaiki na mapato yatokanayo na soka kutokana na klabu kutolipa kodi wakati wa usajili na zinapolipa mishahara wachezaji.
“Juzi juzi klabu ya Yanga ambayo mimi ni shabiki wake, iliripotiwa kumsajili Malimu Busungu kwa dau linalotajwa kuwa Sh. milioni 40, lakini serikali haijapata hata milioni tano katika usajili huo,” amesema.
“Baadhi ya wachezaji wanalipwa mishahara madirishani. Ni changamoto mchezaji wa ligi kuu hana hata akaunti benki,” amaesema.
Hata hivyo, mwenyekiti wa zamani wa kilichokuwa Chama cha Soka Tanzania (FAT sasa TFF), Muhidin Ndolanga, ameoneshwa kuguswa na suala hilo na kumjibu moja kwa moja jukwaani Mtanda kuwa serikali imeshindwa kusimamia sheria zake za kodi.
“Kama wachezaji hawakatwi kodi, maana hakuna sheria inayowalazimisha kufanya hivyo. Inabidi kuwa na ulazima wa kulipa kodi na kuchangia kwenye mifuko ya kijamii kwa maisha ya baadaye ya wachezaji.
0 comments:
Post a Comment