728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 04, 2015

    MILNER ATUA LIVERPOOL,BENITEZ AAPA KUIBOMOA ARSENAL

    Habari na Paul Manjale

    Milner:Klabu ya Liverpool mapema leo imetangaza kumnasa kiungo James Milner 29 akiwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake katika klabu ya Manchester City. kwa uhamisho wa bure.Milner atakuwa akivuna kitita cha £150,000 kwa wiki.
                                    
    Koscielny:Kocha mpya wa klabu ya
    Real Madrid Raphael Benitez amewataka mabosi wa klabu hiyo kufanya kila wawezalo kuhakikisha wanamsajili mlinzi wa kati wa klabu ya Arsenal. Laurent Koscielny ili kukisuka upya kikosi chake katika idara ya ulinzi.
                                   
    Kondogbia:Klabu ya Arsenal omeripotiwa kupeleka kitita cha £25.7m kwa ajili ya kumsajili kiungo wa klabu ya Monaco Geoffrey Kondogbia,22.Wakati huohuo kiungo wa Southampton Victor Wanyama ameiambia klabu ya Arsenal kuwa yuko tayari kujiunga nayo katika kipindi hiki cha usajili.
                                  
    Ferrero:Raisi wa klabu ya Palermo ya Italia Massimo Ferrero amesema klabu yake iko katika mazungumzo na klabu ya Chelsea kwa ajili ya kumsajili mlinzi Kurt Zouma.Ferrero ameyasema hayo wakati akimtambulisha nyota mpya wa klabu hiyo kutoka Ajax  aitwaye Moisander.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MILNER ATUA LIVERPOOL,BENITEZ AAPA KUIBOMOA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top