728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 04, 2015

    NOOIJ ATANGAZA 23 WATAKAOWEKA KAMBI ETHIOPIA

    Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 23 watakaoondoka leo jioni kuelekea Addis Ababa nchini Ethiopia kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri

    Akiongea na waandishi wa habari, kkocha Mart Nooij
    amesema watatumia kambi ya Ethiopia kujiandaa na mchezo wa Misri, vijana wapo katika hali nzuri na wameahidi kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo.
    Mchezo kati ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa Juni 14, katika uwanja wa Borg El Arab jijini Alexandria, ikiwa ni mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwaka  2017.
    Kikosi cha Stars kinaondoka saa 11 jioni kwa Shirika la ndege la Ethiopia ambapo inatarajiwa kuwasili jiji la Addis Ababa majira ya saa 1 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
    Wachezaji wanaosafiri kuelekea nchini Ethiopia ni  Deogratias Munish, Aishi Manula, Mwadini Ali, walinzi Shomari Kapombe, Oscar Joshua, Erasto Nyoni, Nadir Haroub, Aggrey Morris, Mwinyi Haji, Salum Mbonde na Juma Abdul.
    Wengine ni Mwinyi Kazimoto, Abdi Banda, Salum Telela, Frank Domayo, Jonas Mkude, Said Ndemla, washambuliaji Saimon Msuva, John Bocco, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta,Mrisho Ngasa na Juma Liuzio.
    Msafara wa Taifa Stars utaongozwa na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji, Vedastus Lufano na Geofrey Irick Nyange “Kaburu”.
    Naye mjumbe wa kamati ya Utendaji  ya TFF Vedastus Lufano amesema timu inakwenda kuweka kambi Ethiopia kwa ajili ya kupambana katika mchezo dhidi ya Misri.
    Kikosi kingine cha timu ya Taifa kitaondoka nchini siku ya jumamosi kuelekea nchini Rwanda kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya Rwanda katika kumbukumbu ya mauaji ya Kimbali.
    Kocha Salum Mayanga ataondoka na kikosi cha wachezaji 18 kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo huo wa kirafiki, akisaidiwa na kocha Bakari Shime.
    Wachezaji watakaondoka kwenda Rwanda ni Peter Manyika, Said Mohamed, Emmanuel Semwanda, Joram Mgeveke, Hassan Isihaka, Gadiel Michael, Hassan Dilunga, Rashid Mandawa, Atupele Green, Kelvin Friday, Hassan Kessy, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu, Mudathir Yahya, Deus Kaseke, Andre Vicent, Amri Kiemba na Mohamed Hussein.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: NOOIJ ATANGAZA 23 WATAKAOWEKA KAMBI ETHIOPIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top