728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, June 05, 2015

    TETESI ZA USAJILI MAJUU:MAN UTD YAMSAKA MRITHI WA DE GEA

    Habari na George James

    Muslera:Man u wanafikiria kumsajili golikipa namba moja club ya Garatasaray Fernando Muslera kwa ajili ya kuziba nafasi ya De Gea anayeelekea Madrid (source metro)

    Advocaat:Kocha wa Sunderland
    Dick Adivocaat anafikiria kutumia kiasi cha pauni 50m ili kuboresha kikosi chake kwa kuwasajili Virgil van dijk,Patrick Bamford,Seko Fofana ,Sam,Byram na Sebastian Coates(daily express)

    Falcao:Mshambuliaji wa timu ya taifa wa Colombia radamel Falcao Garcia El tigre amesema anataka kukamilisha dili lake la kujiunga na mabingwa wapya wa epl chelsea fc kabla ya kuanza kwa michuano ya copa america (Daily telegraph)

    Dante:Beki wa Bayern Munich Dante amesema anataka kubaki Bavarians baada ya hapo jana kuwepo tetesi za yeye kutakiwa na mashetani wekundu Man Utd (Daily star)

    Nani:Man utd wanafikiria kumuuza winga wao aliye kwa mkopo Luis Nani na timu pekee iliyotayari kumsajili ni Inter Milan ya Italy kwa dau la paun 7m (The independent)

    Zouma:Sampdoria nao wanafikiria kumsajili beki wa chelsea fc Kurt Zouma kwa mujibu wa raisi wa club yao ( Metro)

    Wanyama:Victor Wanyama kasema itakuwa vizuri yeye akijiunga na mabingwa wa kombe la Fa the gunners(Daily mail )

    Kondogbia:Arsenal wanafikiria kupeleka dau la paun 25 m kwa kiungo wa monaco Geoffrey Kondogbia ikiwa watamkosa kiungo wa Soton Morgan Schneiderlin (the independent)

    Alves:Man utd yaendelea kuipa pigo Liverpool kwa kufanya mazungumzo ya awali na Dani Alves ambaye alikuwa pia akitakiwa na Liverpool hii inakuja siku si nyingi baada ya Man U kuwazidi kete majogoo hao kwa kumsajili winga wa Psv Endhoven Memphis Depay(Daily star)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TETESI ZA USAJILI MAJUU:MAN UTD YAMSAKA MRITHI WA DE GEA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top