Bejaia,Algeria.
Timu ya Yanga imeanza vibaya mechi zake za makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) baada ya kufungwa bao 1-0 na MO Bejaia huko Algeria.
Bao hilo lililoizamisha Yanga lilifungwa dakika ya 20 na Yacine Sahli, katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia Jumatatu.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na waamuzi kutoka Morocco, Amissi Tambwe alishindwa kufurukuta na kutolewa kumpisha Simon Matheo ambaye hata hivyo hakusaidia Yanga kuepuka kipigo hicho.
0 comments:
Post a Comment