728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 04, 2016

    KOCHA ALGERIA ABWAGA MANYANGA

    Algers, Algeria. 

    Christian Gourcuff amebwaga manyanga kuifundisha timu ya taifa ya Algeria (The Desert Foxes).

    Taarifa kutoka katika mtandao wa chama cha soka cha Algeria zimesema Kocha huyo Mfaransa ameomba kwa hiari yake kusitisha kuifundisha Algeria na tayari aliyekuwa msaidizi wake Nabil Neghiz ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa muda.

    Hakuna sababu rasmi iliyotolewa juu ya uamuzi huo wa Gourcuff wa kuitema Algeria ingawaje ingawaje kuna habari kuwa kocha huyo anakwenda kujiunga na klabu ya Bordeaux inayoshiriki ligi daraja la kwanza Ufaransa.

    Gourcuff aliteuliwa kuifundisha Algeria Agosti 2014 akichukua nafasi ya Mbosnia Vahid Halilhodzic. 

    Akiwa na Algeria Gourcuff aliiwezesha miamba hiyo ya Afrika Kaskazini kufuzu michuano ya Afcon 2015 huko Afrika Kusini na kuishia hatua ya robo fainali baada ya kufungwa 3-1 na Ivory Coast.

    Wakati huohuo Taarifa kutoka Algeria zinasema tayari chama cha soka cha nchi hiyo FAF kimeanza mipango ya kuziba nafasi ya Gourcuff kwa kufungua mazungumzo na makocha Marcello Lippi wa Italia na Marcelo Bielsa wa Argentina.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: KOCHA ALGERIA ABWAGA MANYANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top