Cairo, Misri.
WANAJUA!!Wapinzani wa Yanga katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Al Ahly (Red Devils) ya Misri wameendelea kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo baada ya jana jumapili kuichapa Ittihad El-Shorta Kwa mabao 5-3.
Al Ahly ambayo jumamosi ijayo itakuwa Uwanja wa Taifa kuvaana na Yanga imepata ushindi huo mkubwa kwa mabao ya Momen Zakaria (17),Ahmed Fathi (22 na 45) ,Mohamed Abdel-Salam aliyejifunga (44) na Amr Gamal (78)
Ittihad El-Shorta wamepata mabao yao kupitia kwa Salah Rico aliyefunga kwa mkwaju wa penati na Abdulaye Cisse aliyefunga mara mbili.
0 comments:
Post a Comment